RIDHIWANI KIKWETE AANZA KUPIGA HESABU ZA BUNGENI
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete.
Bagamoyo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani
Kikwete ameanza kujinadi akisema endapo ataingia bungeni, atawaelimisha
wabunge juu ya kuweka mbele maslahi ya Watanzania badala ya kulalamikia
posho.
Ridhiwani
ambaye juzi alithibitishwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea wa jimbo
hilo lililowahi kuongozwa na baba yake, Jakaya Kikwete alisema kitendo
cha kutumia muda mwingi kubishania kanuni na wengine kulalamikia posho
kinatia aibu kwani Watanzania wanahitaji Katiba Mpya.
Alisema
hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya
kuwania ubunge wa jimbo hilo katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo.
Ridhiwani
alisema, ikiwa atapata fursa ya kuingia bungeni, atawaelimisha wabunge
wa Katiba ili waweze kuangalia maslahi ya wananchi kwanza na si kugombea
posho.
Alisema,
kitendo kinachotokea kwenye Bunge Maalumu la Katiba cha wajumbe kugombea
posho kinatia aibu, hivyo basi wanapaswa kuelimishwa, ili waweze kujua
wajibu wao.
Ridhiwani alisema kinachoonekana katika Bunge hilo ni kutunishiana misuli na si kuangalia maslahi ya wananchi,
Kutokana na hali hiyo, alisema wajumbe hao wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo na kuangalia maslahi ya wananchi.
waliowawakisliha pale, na si kuangalia mambo yao binafsi, jambo ambalo linaweza kuongeza migogoro.
Chanzo, mwananchi
RIDHIWANI KIKWETE AANZA KUPIGA HESABU ZA BUNGENI
Reviewed by crispaseve
on
00:17
Rating:
Post a Comment