Washiriki kutoka Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda wako Moro
Mwandishi Wetu, Dar es alaam
WASHIRIKI wa shindano la Maisha Plus ambayo kwa mwaka 2014 inatambulika
kwa jina la Maisha Plus Rekebisha, kutoka nchini Kenya, Rwanda,Uganda na
Burundi tayari wameshawasili nchini na jana wameelekea wako mkoani
Morogoro kushiriki shughuli za kijamii.
Mratibu wa onyesho hilo, Ally Masoud Kipanya amesema hili ni kundi la
tatu kushiriki shughuli za kijamii, ambapo kundi la kwanza lilikuwa
Iringa, kisha la pili likaenda Zanzibar na hili la tatu linaenda
Morogoro kushiriki shughuli za kijamii, huku lengo kubwa likiwa ni
kubadilisha maisha ya wanajamii wa huko.
"Hii ndio sababu Maisha Plus ya mwaka huu inaitwa Maisha Plus Rekebisha,
ambapo lengo kuu ni kuangalia matatizo ya eneo husika na kuangalia
jinsi ya kutatua, na sio kulalamika, tunataka kurekebisha wananchi wenye
fikra za kusubiri kufanyiwa, kuwa wepesi wa maamuzi na kutatua matatizo
waliyonayo", alisema Masoud
“Wananchi wengi hulalamikia serikali juu ya maswala mbalimbali ambayo
hata wao wenyewe wanaweza kuyarekebisha bila kusubiri
kufanyiwa”,alisema.
Washiriki kutoka nchi jirani ni walio mkoani Morogoro kwa sasa ni
Loveness Asantely ,Mary Sidi(kutoka Kenya), Borandanginye Aurore, Mvano
Ciza, na Abdou Karim(kutoka Burundi), Aminata Siira(kutoka Uganda),
Uwamahoro Fatima, Ngabozinza Khalid, na Ngabozinza Daniel (kutoka
Rwanda)
Kupitia Maisha Plus Rekebisha mwaka huu, wananchi watapata elimu juu ya
kuepukana na mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo magonjwa kama
malaria, kipindupindu, homa ya manjano na mengineyo.
Washiriki wote kwa ujumla kutoka nchi za jirani wanatakiwa kuwa 12
nambili,waliofika nchini ni 10 wawili wanaotambulika kwa majina Said
Rashid (Uganda) na Caron Abisai (Kenya) bado hawajafika.
Washiriki kutoka Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda wako Moro
Reviewed by crispaseve
on
00:42
Rating:

Post a Comment