YANGA YAFUNGASHIWA VIRAGO NA WAARABU
Timu
ya Yanga SC imeondolewa kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika
baada ya kufungwa na Al Ahly kwa penalti 4-3 katika mechi iliyochezwa
Uwanja wa El Max Haras El Hodod jijini Alexandria, Misri!
Mpaka
dakika ya 90 ya mchezo, matokeo ya jumla yalikuwa 1-1 hivyo kuamriwa
kupigwa mikwaju ya penalti ambapo Yanga walipata 3, wakati Al Ahly
wakipata 4.
Wachezaji
wa Yanga waliofunga penalti ni Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi na Nadir
Haroub 'Cannavaro' wakati Oscar Joshua, Mbuyu Twite na Said Bahanuzi
wakikosa mikwaju hiyo.
Kwa matokeo hayo, timu ya Al Ahly imefuzu katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
(PICHA NA SALEH ALLY / GPL, ALEXANDRIA)
Al Ahly wanapata penati 4 - 3 Young Africans
Waliopata Yanga Didier, Canavaro, Okwi huku waliokosa ni Oscar, Bahanuzi na Twite Al ahly wanafuzu hatua ya 16 bora
YANGA YAFUNGASHIWA VIRAGO NA WAARABU
Reviewed by crispaseve
on
15:19
Rating:
Post a Comment