MUENDELEZO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO HUKO UGHAIBUNI
Katika
kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
Timu ya Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya
Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi
walihudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba ambae ni
Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa
Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa
nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi
Zanzibar. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)

Naibu
Mwakilishi Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa mataifa New York,
Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia) akiwa pamoja na Viwe Juma, ambae ni
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya BENKI ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) ambao ni wadhamin wa timu hiyo wakimkabidhi jezi nahodha
wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein Siku ya Jumamosi April 26,
ndani ya Ubalozi wa Tanzania jiji Washington DC nchini Marekani, ili
kujianda kupambana na timu ya Kilimanjaro Stars kwa mchezo wa kuwania
Kombe la Muungano.
Viongozi:
Wageni rasmi wa sherehe za Muungano Mhe: Mwigulu Nchemba (wapili
kulia) akifuatiwa na Balozi Mulamula, pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi
Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, (wakwanza
kulia) Viwe Juma,wapili kulia ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na
Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimkabidhi
jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein katika Sherehe za
Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye ubalozi wa
Tanzania uliopo Jijini Washington DC.

Wasimamizi wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir na Dedie Rouba wakionyesha jezi walizodhaminiwa na (PBZ) Benki ya Watu wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe Juma akipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe Juma akipata picha ya pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night.
Mwenyekiti
wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali akipata picha ya pamoja
na mgeni ndani ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC
Nchini Marekani
Miss Tanzania USA akipata picha ya pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night
MUENDELEZO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO HUKO UGHAIBUNI
Reviewed by crispaseve
on
05:13
Rating:
Post a Comment