Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima
Frank Mvungi
SERIKALI
imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima
katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo kwa wakulima baada
ya kuiuzia nafaka Serikali.
Hayo
yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari
leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio
yaliyofikiwa na wakala huo.
Walwa
alisema kuwa wakala huo umeweza kuongeza kiasi cha nafaka
zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka tani 61,587.784 mwaka
2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni matokeo ya
kuboreshwa kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.
“Hadi
kufikia Desemba 31 mwaka 2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za
nafaka sawa na asilimia 110 ambapo tani 218,878.600 ni mahindi na tani
498.682 ni mtama” alisema Walwa.
Aliongeza
kuwa wakala umeingia makubaliano ya mashirikiano ( Memorandum of
Understanding(MOU) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili
kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.
Katika
kutekeleza makubaliano na WFP Walwa alisema kuwa wakala umeuza tani
80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa wakala unaendelea kutekeleza
mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka 2013/2014.
Katika
hatua nyingineWalwa alisema kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya
nafaka kutoka kwa wananchi, ajira za muda kwa wananchi takribani 3000
zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakati wa kukusanya
nafaka tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula umepanga kuongeza uwezo wa kuhifadhi
nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa hadi tani laki 400,000 ifikapo mwaka
2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.
Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima
Reviewed by crispaseve
on
05:09
Rating:

Post a Comment