TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA VIVINJARI VYA “INERNET EXPLORER”
Mwishoni
mwa juma pamegundulika hali mbaya ya kiusalama mtandao itakayo waathiri
watumiaji wa kivinjari kijulikanacho kama "internet explorer" ambapo
watumiaji wa kivinjari hicho wako hatarini kuweza kuingiliwa kirahisi
computer zao na wahalifu mtandao.
Jumamosi
tangazo hilo linalosomeka hapa "TANGAZO" limeweza kubainisha internet
explorer toleo la 6 hadi la 11 yote yameweza kugundulika yanatoa mwanya
kwa wahalifu mtandao kupenya kwa watumiaji na kuchukua taarifa zozote
zitakazo patikana kwenye computer zao.
Aidha,
Kampuni inayo jihusisha na na maswala ya ulinzi mtandao ya "FireEye"
imeonyesha takwimu yakua asilimia 56 ya vi vinjari kwa hadi ilipofikia
mwaka 2013 vilikua hatarini kuingiliwa na wahalifu. na kubainisha kwamba
wahalifu wamekua na uwezo wa kutengeneza vivinjari visivyo sahihi
vinavyo weza ruhusu wahalifu hao kuingilia computer za watu mara tu
watumiaji wa vi vinjari hivyo wanapo vitumia.
Microsofti
imeshindwa kupata suluhu ya tatizo hilo ambapo CERT ya marekani imetoa
tahadhari linalosomeka hapa "CERT ALERT" yakuwa watumiaji vivinjari vya
"internet explorer" wanapaswa kubadil vivinjari kwa sasa na badala yake
watumie vingine hadi hapo tatizo litakapo rekebishwa na kutangazwa
vingenevyo.
Aidha,Christian
Tripputi Ametumia muda huu kuonya watumiaji wa Window XP yakuwa kwa
sasa wako hatarini kwani hakuna tena huduma zitakazo endelea kutolewa
kwa Window hiyo na wahalifu mtandao wamesha anza kuleta madhara kwa wote
wanaoendelea na matumizi ya windo hiyo na kusisistiza hapata kuwa na
msaada kwa waathirika. Taarifa ya awali ilyotelewa na Yusuph kileo
kuhusiana na matumizi ya Window XP inasomeka hapa “TAHADHARI KWA
WATUMIAJI WA WINDOW XP".Crdt Michuzi Blog
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA VIVINJARI VYA “INERNET EXPLORER”
Reviewed by crispaseve
on
04:57
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
04:57
Rating:



Post a Comment