Timu 72 kushiriki Ester Cup 2014, mshindi kupata sh 1.5 million
Jumla
ya timu 72 zitashiriki katika mashindano ya soka ya Ester Cup ambayo
huandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, kwa tiketi ya vijana
wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ester Bulaya. Mashindano
hayo, yanafanyika mwaka huu kwa msimu wa nne katika Jimbo la Bunda, na
yatachukua nafasi katika viwanja vya Sabasaba, Shule ya Msingi Bunda,
Nyamswa na Mgeta.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini jana (leo), Bulaya alisema kuwa
mashindano hayo yamekuwa kulinganisha na miaka ya nyuma. Alisema kuwa mwaka 2011 jumla ya timu 18 zilishiriki, mwaka 2012 timu 26 wakati mwaka jana ziliongezeka mpaka 38. Bulaya alisema, ameamua kuendeleza mashindano hayo ili iwe fursa ya ajira kwa vijana wenye vipaji vya soka.
“Mimi
ni mzaliwa wa Bunda na moja ya changamoto za jimbo letu ni kutokuwa na
mashindano ya soka, nilipoanzisha mashindano ya Ester Cup nilileta
kuhamasisha michezo jimboni kwetu, nafurahi kwa sasa lengo limetimia na
hamasa katika jimbo hilo imeongezeka,” alisema Bulaya.
Alisema,
tangu kuanza kwa mashindano, wilaya ya Jimbo la Bunda na wilaya nzima
ya Bunda, imepata mafanikio makubwa na wachezaji wengi wamepata ajira
kwenye klabu mbalimbali kubwa zinazoshiriki michuano mikubwa nchini.
Alifafanua
kuwa ili kuleta maendeleo katika michuano hiyo, wamezuia wachezaji nje
ya jimbo la Bunda kucheza Ester Cup jambo ambalo halitasaidia malengo
yetu ya kuendeleza michezo kwa vijana wa jimbo husika.
Bulaya
alisema kuwa jumla ya Sh15.4 zimetumika kugharimia mashindano ya
mwaka ambapo mshindi atapata Sh 1.5 million ambapo mshindi wa pili
atazawadiwa Sh700,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa Sh 500,000.
Aliongeza
kuwa pia amefanikiwa kugawa vifaa mbali mbali kwa wilaya nne na kata
150 za wilaya nne, shule za sekondari na kutumia jumla ya Sh 75 million.
Alisema kuwa wilaya ya Rorya na Tarime pekee ndizo hazijapata msaada
huo na yupo mbioni kuwakabidhi.
Timu 72 kushiriki Ester Cup 2014, mshindi kupata sh 1.5 million
Reviewed by crispaseve
on
15:59
Rating:

Post a Comment