ZIARA YA SADIFA YATIKISA KATA YA KAWE
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto)
akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar
es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano
wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka
katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian
Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.
Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani
Naibu
Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano
wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe
Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa
kuhutubia.
Mwenyekiti
wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa
UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye
Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku
shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe,
Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.
Sadifa akigawa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya soka ya Ukwamani Shooting, wakati wa mkutano huo
Mlezi
wa UVCCM Kata ya Kawe, Coolman Massawe, akikabidhi vifaa vya michezo
kwa kiongozi wa timu ya Ukwamani, Ali Kidogodogo, wakati wa mkutano huo.
ZIARA YA SADIFA YATIKISA KATA YA KAWE
Reviewed by crispaseve
on
05:42
Rating:
Post a Comment