CHINA NA TANZANIA ZATILIANA SAINI MKATABA WENYE THAMANI YA DOLA LAKI MOJA ZA KIMAREKANI
Katibu
wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah
akitoa maelezo juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Bunge la Jamhuri la
Muungano wa Tanzania leo wakati wa sherehe fupi ya utiaji saini mkataba
wathamani ya dola laki moja za kimarekani kati ya Chama cha Kupunguza
matumizi ya silaha na Maridhiano cha China na Ofisi za Bunge la Jamhuri
la Muungano wa Tanzania.
Baadhi
ya viongozi toka pande zote mbili wakiwa katika sherehe ya utiaji saini
mkataba wa thamani ya dola laki moja za kimarekani kwaajili ya ununuzi
wa vifaa vya ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania
uliofanyika leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah
(kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya
Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’
Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan wakitia saini
mkataba huo wa thamnai za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi
ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.

(kulia) akimkabidhi zawadi mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China
(Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen
Huaifan (kushoto) mara baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano wenye
thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge
zilizopo jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Na. Benedict Liwenga-MAELEZO.
16/05/2014
OFISI
ndogo ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo imetialiana saini
na Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya
Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament)
wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.
Utaiji
saini huo umefanyika leo katika Ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ukihusisha viongozi wa pande zote mbili akiwemo
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah
pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha
na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association
for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah
amesema kuwa mkataba huo wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani
utasaidia ofisi ya Bunge kuweza kupata vifaa mbalimbali vya ofisi
vikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu, vipaza sauti, kamera pamoja na
vifaa vya kurekodia.
“Ndugu
zetu kutoka China pamoja na hiki Chama chao wamesaini pamoja nasi
mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani ambao wametutaka
sisi tuamue wenyewe ni vifaa gani tunahitaji kwaajili ya ofisi yetu ya
Bunge mjini Dodoma ili wao waweze kutununulia na kutukabidhi”. Alisema
Kashililah.
China
na Tanzania zimekuwa zikitiliana saini mikataba mbalimbali ya maendeleo
ambayo kwa namna moja mikataba hiyo imekuwa ikizinufaisha pande zote
mbili kiuchumi na mpaka hivi sasa uhusiano huu umedumu kwa muda miaka
hamsin
CHINA NA TANZANIA ZATILIANA SAINI MKATABA WENYE THAMANI YA DOLA LAKI MOJA ZA KIMAREKANI
Reviewed by crispaseve
on
02:34
Rating:

Post a Comment