CHRIS BROWN KUSHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA JELA
Upepo
mbaya bado umeendelea kumuandama mwimbaji wa kibao cha Loyal ‘Chris
Brown’ ambaye kwa hivi sasa anasotea nyuma ya nondo za jela baada ya
upande wa utetezi kubainisha ya kwamba huenda staa huyo akasherekea siku
yake ya kuzaliwa akiwa ndani.
Hiyo inakuja kufuatia jaji Brandlin kutupilia mbali ombi la
kupewa dhamana kwa mwanamuziki huyo na kuamuru aendelea kukaa ndani
walau kwa wiki moja zaidi mpaka pale tamko juu ya kesi yake dhidi ya
Rihanna litakapokubaliwa baina ya mwendesha mashitaka na wakili wa
nyota huyo ‘Mark Geragos’ kabla ya muda wa kusikilizwa kwa kesi hiyo
uliopangwa kufanyika Mei 09 mwaka huu.
Halikadhalika mwimbaji huyo anaweza akakumbana na adhabu ya
kifungo cha miezi sita au zaidi jela endapo atakutwa na hatia ya kesi
iliyokuwa inamkabili mwaka jana ya kumshambulia mtu mmoja nje ya hotel
ya W iliyopo jijini Washington Dc marekani.
CHRIS BROWN KUSHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA JELA
Reviewed by crispaseve
on
01:57
Rating:

Post a Comment