Header AD

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI BABATI,KESHO KUUNGURUMA WILAYANI KITETO MKOANI MANYARA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wananchi,katika mkutano wa hadhara wakati akihitimisha ziara yake katika wilaya ya Babati,mkoani Manyara. Mkutano huo umefanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati,ukihudhuriwa na maelfu ya Wananchi.Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,kwenye ziara ya siku saba mkoani Manyara,ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Maelfu ya Wananchi wa mjini Babati wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana aliwahutubia Wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi jioni ya leo kwenye uwanja wa Kwarahaa,wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Babati .
  Katibu wa CCM,Ndugu Kinana akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt.Daniel Mbwambo (wa pili pichani kulia),ambaye pia ni Meneja wa Maabara katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.Shoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara,Injinia Omar Chambo
 Pichani Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara,Injinia Omar Chambo,akizungumza  mbele ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo ,Katibu Tawala mkoa wa Manyara,Injinia Omar Chambo amesema kuwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye hospitali ya Kilutherii ya Haydom wilayani Mbulu imezaa Matunda,kufuatia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kumtaarifu kuwa anatakiwa kuwaajiri watumishi 93 wa hospital hiyo,ambao walikuwa wanahamia serikalini katika hospitali mbalimbal,hivyo wanaingizwa katika utaratibu wa ajira ya serilali na wanatakiwa kubaki hospitalini hapo kwa utumishi wao.

Aidha Serikali katika utaratibu wake wa ruzuku,imeiongezea ruzuku hospitali hiyo inayofadhiliwa  na nchi ya Sweden kwa miaka 50,kutoka shilingi milioni 200 mpaka milioni 320 kwa mwaka ili kuboresha zaidi huduma za hospitali hiyo,ambayo imekuwa ikihudumia zaidi ya mikoa sita ya kaskazini na kanda ya kati.
 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara jioni ya leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua madarasa ya shule ya sekondari ya Kamoto wilayani Babati mapema leo.
 Kinana akikagua moja ya nyumba ya waalimu shule ya sekondari ya Kamoto wilayani Babati.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya Maji mkazi wa Kijiji cha Himiti Kata ya Bonga, wilaya ya Babati mjini, Zena Rashid, baada ya kuzindua mradi wa maji wa kata hiyo leo akiwa katika katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya hiyo ya Babati mjini mkoani Manyara. 
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo.
 Sehemu  ya Wananchi wakifautilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara mjini Babati
KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI BABATI,KESHO KUUNGURUMA WILAYANI KITETO MKOANI MANYARA KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI BABATI,KESHO KUUNGURUMA WILAYANI KITETO MKOANI MANYARA Reviewed by crispaseve on 01:30 Rating: 5

No comments

Post AD