Header AD

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KITUO CHA TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA NA SARATANI ZA MATUMBO NA INI CHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, JIJINI DAR LEO.

1 (4) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) Mwakilishi wa Taasisi ya Else Kronner Fresenius Stiftung, Prof. Konrad Mebmer (wa tatu kushoto) Mwenyekiti wa Mfuko wa Magonjwa ya mfumo wa Chakula Munich nchini Ujerumani, Prof. Meinhard Classen (kulia) na Balozi mdogo wa Ujerumani nchini Tanzania, Hans Koeppel, kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kufungua rasmi Jengo la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa Hafla fupi ya ufunguzi huo iliyofanyika Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014.
01 (3)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa Hafla fupi ya ufunguzi huo iliyofanyika Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014. 
2 (4)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Prof. Leonard Lema (wa pili kulia) kuhusu Mashine ya kuchunguza mfumo wa Hewa na Chakula, wakati Makamu alipokuwa akitembelea jengo jipya  la Kituo cha Tiba, Uchunguzi na Mafunzo ya Magonjwa na Saratani za Matumbo na Ini cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujionea mashine hizo, leo Mei 30, 2014. (wa pili kushoto) ni Mtaalam wa mfumo wa chakula, Edwaldo Komba. 
4 (2)Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia baada ya kufungua rasmi jingo hilo. Picha na OMR
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KITUO CHA TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA NA SARATANI ZA MATUMBO NA INI CHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, JIJINI DAR LEO. MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KITUO CHA TIBA, UCHUNGUZI NA MAFUNZO YA MAGONJWA NA SARATANI ZA MATUMBO NA INI CHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, JIJINI DAR LEO. Reviewed by crispaseve on 01:28 Rating: 5

No comments

Post AD