Header AD

Kamati Tendaji ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, yazuru Kibaha, Pwani.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kwa walengwa wa Mpango huo (hawapo pichani).

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Tatu Seleman (mwenye miwani) akiangalia moja ya mikeka iliyosukwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini,PSSN, katika kijiji cha Vikuge kama njia mojawapo ya kukuza kipato cha wananchi.
 Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Vikuge wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wakiwa katika mkutano uliohudhuriwa pia na wajumbe wa kamati tendaji ya TASAF (hawapo pichani) iliyotembelea kijiji hicho kukagua shughuli za Mpango huo zinavyoendelea.
 Karibu wageni hivi ndivyo anavyoelekea kusema Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza(aliyeko mbele ya wajumbe) wakati alipowakaribisha wajumbe wa kamati tendaji ya TASAF iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea vijiji vya Vikuge na Misufini kukutana na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini ,PSSN.
 Kaimu mwenyekiti wa kamati tendaji ya TASAF Abbas Kandoro (katikati) akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (aliyevaa kilemba) wakati wajumbe wa kamati hiyo walipomtembelea mkuu huyo wa mkoa wa Pwani ofisini kwake kabla ya kutembelea vijiji vya Vikuge na Misufini katika wilaya ya Kibaha kukaguwa shughuli za walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF,kushoto kwa Kandoro ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga
Kamati Tendaji ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, yazuru Kibaha, Pwani. Kamati Tendaji ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, yazuru Kibaha, Pwani. Reviewed by crispaseve on 01:23 Rating: 5

No comments

Post AD