Header AD

MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA EPL, WAILAZA 2 – 0 WESTHAM, LIVERPOOL YAITUNGUA 2 – 1 NEWCASTLE



Manchester CityHatimaye kikosi cha Manchester City kilicho chini ya kocha mkuu ‘Manuel Pellegrini’  kimeweza   kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England maarufu kama EPL baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2 – 0 dhidi ya wagonga nyundo wa jiji la London Westham United katika mtanange  wa mwisho wa kufunga pazia la ligi kuu hiyo inayoongoza kwa kutazamwa na wapenzi wengi wa soka  Duniani.
PellegriniWachezaji wa Manchester City wakiwa wamemnyanyua juu kocha wao Manuel Pellegrini ikiwa ni ishara ya kuonyesha ni jinsi gani walivyokuwa na furaha
Mabao ya City yalifungwa na Samir Nasir baada ya kupewa pasi nzuri kutoka kwa  kiungo mshambuliaji Yaya Toure huku goli la pili likifungwa na Vicent Kompany. Mchezo mwingine uliokuwa wa vuta nikuvute ni ule ulioikutanisha klabu ya Liverpool waliowakaribisha nyumbani NewCastle United ambao walikubali kipigo cha bao 2 -1 kutoka kwa majogoo hao wa London  katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Anifield jijini humo.
Manchester City FunsMagoli ya Liverpool yalifungwa kupitia mshambuliaji wake hatari  Daniel Sturridge pamoja na Daniel Agger  aliyesawazisha huku  bao pekee la kufutia machozi kwa Newcastle likipatikana baada ya mchezaji wa Liverpool Martin Skrtel kujifunga  wakati akijaribu kuokoa mpira.
Warm welcome: The home support git right behind their team from the start of Liverpool vs Newcastle
Wachezaji wa Liverpool wakiwa wamekosa furaha licha ya ushindi wa bao 2 -1 dhidi ya NewCastle lakini haikuwa muarobani kwa Man City walioibuka mabingwa
Matokeo hayo yameiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa huo mkubwa kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu wa mwaka 2011/12 pamoja na 2013/14 huku ikimaliza  kileleni mwa  ligi hiyo kwa jumla ya pointi 86,  wakati wapinzani wao wanaowafuatia ‘Liverpool’ wakiwa nyuma  yao kwa tofauti ya pointi mbil tu huku  Norwich City, Fulham pamoja na Cardiff zikijikuta zikishuka daraja.
battle cry: The Liverpool fans were in fine voice ahead of facing Newcastle in the final game of the season
mashabiki wa Liverpool wakiishangilia timu yao
Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na Cardiff iliyokubali kipigo cha bao 1 -2 toka kwa Chelsea, Fulham ikitoka sare ya 2 – 2 na Crystal Palace wakati Norwich ikiloweshwa goli 0 – 2 kutoka kwa washika mtutu wa jiji la London ‘Arsenal, Southampton ikiilzamishana sare ya bao 1 – 1 na Manchester United, Sunderland wakichezea bao 1 – 3 toka kwa Swaswea City, Tottenham Hotspurs ikiigalagaza 3 -1 Aston Villa na mwisho kabisa ni West bromwich Albion iliyopokea kipigo cha 1 – 2 toka kwa Stoke City.

MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA EPL, WAILAZA 2 – 0 WESTHAM, LIVERPOOL YAITUNGUA 2 – 1 NEWCASTLE MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA EPL, WAILAZA 2 – 0 WESTHAM, LIVERPOOL YAITUNGUA 2 – 1 NEWCASTLE Reviewed by crispaseve on 01:04 Rating: 5

1 comment

Post AD