Picha Maalum Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Tazama Matukio Mbalimbali ya Ziara ya Kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe nchini Uturuki
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
akisalimiana na Naibu Meya wa jiji la Ankara ambaye naye alikuja Uwanja
wa Ndege kumlaki
Waziri
Membe kushoto akibadilishana mawazo na Balozi wa Uturuki nchini
Tanzania katika Chumba cha Wageni Maalum kwenye Uwanja wa Ndege wa
Ankara
Naibu
Meya wa jiji la Ankara aliyeketi kushoto akibadilishana mawazo na Mhe.
Membe kabala ya kuondoka kutoka katika kiwanja hicho
Waziri
Membe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia anawakilisha
Uturuki aliyekaa kushoto pamoja na Bw. Salvator Mbilinyi, Afisa wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Italia aliyechutama wakibadilishana machache
katika Chumba cha Wageni Maalum ndani ya Uwanja wa Ndege wa Ankara.
Waziri Membe akiendelea kuwahutubia waandishi wa habari hawapo pichani
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe akihutubia Mkutano
wa Waandishi wa Habari huku akimshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uturuki, Mhe. Almet Dovutoglu
Waziri Membe kulia akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Uturuki mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo.
Waziri
Mkuu wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan (kulia) akiwa katika
mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). mazungumzo hayo yalifanyika katika
Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Ankara, Uturuki tarehe 08 Mei, 2014.
Picha Maalum Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Tazama Matukio Mbalimbali ya Ziara ya Kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe nchini Uturuki
Reviewed by crispaseve
on
00:44
Rating:
Post a Comment