MBUNGE MGIMWA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZA MAREHEMU DR MGIMWA AONYA WANAOJIPITISHA
| viongozi wa serikali ya kijiji cha Wangama wakimsikiliza katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga alipofika kukabidhi msaada wa bati 100 na saruji mifuko 50 |
| Katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Martin Simangwa wa tatu kulia akiongoza wananchi wa Wangama kumkumbuka aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu |
Bw Simangwa akizungumza na viongozi wa kijiji cha wangama
|
| Katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Simangwa kulia akikabidhi msaada wa bati kijiji cha Negabihi jana |
Na Francis Godwin Blog
MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa amekabidhi msaada wa bati 280 na saruji mifuko 50 kwa katika kata ya Wangama na Mlanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizozitoa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Dr Wiliam Mgimwa huku akiwataka wananchi kuwapuuza watu wanaojipitisha kutaka ubunge mwaka 2015.
MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa amekabidhi msaada wa bati 280 na saruji mifuko 50 kwa katika kata ya Wangama na Mlanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizozitoa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Dr Wiliam Mgimwa huku akiwataka wananchi kuwapuuza watu wanaojipitisha kutaka ubunge mwaka 2015.
Akikabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni
6.7 jana katibu wa mbunge Mgimwa Martine Simangwa alisema kuwa
mbunge Godfrey Mgimwa ameanza kutekeleza ahadi mbali mbali ambazo
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehem Dr Mgimwa alipata kuzitoa
katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo.
“Mheshimiwa Godfrey Mgimwa mbunge wetu wa jimbo la Kalenga
ameanza kutimiza ahadi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi mbali mbali zilizotolewa na mbunge huyo … hadi
sasa ahadi mbali mbali zimeendelea kutekelezwa na Godfrey Mgimwa kama
alivyopata kuwaahidi wananchi wakati wa kampeni”alisema Simangwa .
Kuwa msaada huo wa bati 100 na saruji mifuko 50 ambao
umetolewa katika kijiji cha Wangama kwa ajili yha ukarabati wa vyumba
vya madarasa katika shule ya Msingi Wangama wakati kijiji cha
Negabihi zimetolewa bati 100 na bati 80 zimetolewa kijiji cha Mlanda
na kuwa zoezi la kukamilisha ahadi mbali mbali za marehem Dr
Mgimwa zinaendelea kutekelezwa katika maeneo yote .
Alisema kuwa hadi mwakani sehemu kubwa ya ahadi hizo
itakuwa imetekelezwa na mbunge Godfrey Mgimwa na kuwataka wananchi
wa jimbo la Kalenga kwa sasa kupuuza wanasiasa wa vyama vya upinzani
na wale wa CCM ambao wameendelea kuzunguka jimboni kwa ajili ya
kuwadanganya wananchi kwa ajili ya mwaka 2014
Simangwa alisema kuwa wapo baadhi ya watu wasiomtakia
mafanikio mbunge Godfrey Mgimwa walipata kuzusha kuwa mbunge huyo
amekamatwa uwanja wa Ndege Dar es Salaam akitaka kukimbilia Uingereza
kuishi jambo ambalo si kweli na wapo ambao walieneza kuwa mbunge
huyo amegoma kuapishwa kwa madai kuwa hataka kuliongoza jimbo hilo.
” Watu hao hao wamekuwa wakieneza uongo kwa wananchi dhidi
ya mbunge Godfrey Mgimwa ila ukweli ni huu mbunge wenu anawapenda
sana na hadi sasa yupo bungeni Dodoma akiendelea na vikao vya bunge
la bajeti na mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho atafanya ziara
hivyo wapuuzeni wote wanaoeneza uongo huo”
Bila kuwataja majina watu hao na vyama vyao alisema kuwa
tayari wameanza kukasilishwa na utekelezaji mzuri wa ahadi mbali mbali
unaofanywa na mbunge Godfrey Mgimwa .
Katibu huyo alisema kwa sasa Mgimwa ni mbunge wa jimbo hilo
wa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama wala dini zao na
kuwa moja kati ya malengo yake ni kugombea tena ubunge mwaka 2015
hivyo kwa kipindi hiki kifupi cha mwaka mmoja uliobaki ni kuona
ahadi zote zilizotolewa na mbunge aliyefariki zinatekelezwa na
kusaidia mambo mengine ya ziada pale yanapojitokeza.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Kalenga mwenyekiti
wa serikali ya kijiji cha Negabihi Gaudence chung’unge alisema
kuwa wao kama wananchi wataendelea kumuunga mkono mbunge huyo na kuwa
hawapo tayari kuwasikiliza wale wanaojipitisha kwa wakati huo.
MBUNGE MGIMWA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZA MAREHEMU DR MGIMWA AONYA WANAOJIPITISHA
Reviewed by crispaseve
on
01:28
Rating:

Post a Comment