DIAMOND AZIDI KUNG’ARA, ATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET AWARDS 2014
Tangu
aweke rekodi ya kuzoa tuzo 7 za KTMA pamoja na kuchaguliwa kuwania Tuzo
za KORA na zile za MTV MAMA, mshika kipaza wa Tanzania ‘Diamond
Platnumz’ ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya
kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuwania Tuzo kubwa kabisa za watu weusi
zinazofahmika kama BLack Entertainment Awards maarufu kama BET huku
akiwa msanii pekee anayetokea Afrika Mashariki.
Katika Tuzo hizo, Diamond anawania kipengele cha ‘Best
International Act’ akichuana vikali na wakali kama vile ‘Davido’
kutoka Nigeria, kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini, Sarkodie wa Ghana,
Tiwa Savage kutoka Nigeria pamoja na Toofan wa Togo.
”KWA SASA SINA MENGI YA KUSEMA,ILA
NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA HATUA HII,NA SIWEZI SAHAU KUWASHUKURU
MASHABIKI WANGU KWA SUPPORT MNAYONIPA NA KUNI MOTIVATE NIZIDI KUFANYA
VIZURI KILA SIKU,NINA IMANI MDA SIYO MLEFU MZIKI WETU UTASOMEKA KWENYE
RAMANI TUNAYOITAKA,NIWAKUMBUSHE TU,HIZI NI NOMINEES HATUA ZA UPIGAJI
KURA ZIKIANZA NITAWAJULISHA.USISAHAU TU KUENDELEA KUNIPIGIA KURA TUZO ZA
MTV MAMA,PIA KORA KWA KULIKE PAGE YAO NA KU COMENT JINA
LANGU.AHSANTENI.” aliandika Diamond kwenye ukurasa wake wa Facebook wenye wafuasi zaidi ya Laki na nusu .
Kilele cha Tuzo za BET ni Jumapili ya June 29 mwaka huu
mjini Los Angels Marekani . KWa pamoja Watanzania tunaweza kumpigia kura
kwa wingi Diamond ili kumuwezesha kunyakua Tuzo hizo zote kubwa
anazowania kwa hivi sasa…
DIAMOND AZIDI KUNG’ARA, ATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET AWARDS 2014
Reviewed by crispaseve
on
06:25
Rating:

Post a Comment