HAWA NDIO WASANII WATAOSHIRIKI KWENYE KILI MUSIC TOUR 2014
Kilimanjaro
premium Lager imeandaa ziara maalumu ya wasanii maarufu kama Kili Music
Tour 2014 ni ziara maalum ya wasanii maarufu zaidi ya wasanii maarufu
zaidi ya 30 ambao watatoa burudani kwenye mikoa isiyopungua 10 hapa
nchini kuanzia Mei hadi Septemba 2014 lengo likiwa ni kupeleka muziki wa
Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.
Wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Diamond, Ommy
Dimpoz, Linex, Proffesor Jay, Izzo Biznes, Kala Jeremiah, Fid Q, Snura,
weusi, ben Pol, Mzee Yusuph, Shilole, Mwasiti, Ney wa Mitego, Mwana FA,
Khadija Kopa, Juma Nature, Warriors From the East, Madee, Young Killer,
Jambo Squad, AY, Vanessa Mdee, Mashujaa Band, Rich Mavoko na Christian
Bella huku Lady Jaydee akitemwa kwenye ziara hiyo licha ya kuchukua Tuzo
hizo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni Tweet ya dharau aliyomjibu shabiki
aliyekuwa akimtaka awe anahudhuria tuzo hizo .


Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari
Meneja
wa Kili, George Kavishe amesema “Hii ni fursa kwa wasanii kuweza
kutambulisha kazi zao katika mikoa hiyo na hatimaye kuongeza fursa kwa
mauzo na kukubalika katika mikoa hiyo”.
Pia katika mikoa itakapofanyika tamasha, wasanii chipukizi
mikoa hiyo watapewa fursa ya kutumbuiza katika utangulizi. Hii ni
kuwajengea uwezo wa kujiamini na pia itakuwa ni jukwaa la kuonyesha
vipaji vyao.
Mikoa itakapopita tuzo itakuwa kama ifuatavyo:
Moshi – Mei 24
Mwanza – Mei 31
Kahama – Juni 7
Kigoma – Juni 14
Iringa – Juni 21
Mbeya – Agosti 9
Dodoma – Agosti 16
Tanga – Agost 23
Mtwara – Agosti 30
Dar es Salaam – Septemba 6.
-kililager.com
HAWA NDIO WASANII WATAOSHIRIKI KWENYE KILI MUSIC TOUR 2014
Reviewed by crispaseve
on
06:28
Rating:

Post a Comment