MASHABIKI 15 WAFARIKI DUNIA KWENYE MECHI YA TP MAZEMBE NA AS VITA NCHINI CONGO
Mashabiki 15 wa soka wamekufa kwa kukanyagana baada ya polisi
kufyatua mabomu ya kutoa machozi kwenye kundi la watu kwenye uwanja wa
soka wa Stempede uliopo katika jiji la Kinshasa, jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi nchini humo wamesema mashabiki walipatwa na hasira jana jioni baada ya timu yao ya AS Vita Club kuchapwa kwa bao moja kwa sifuri na klabu ya Tp Mazembe toka mji wa Lubumbashi .

Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza na kikosi cha msalaba mwekundu
Kiongozi mmoja wa mjini huko ‘Emmanuel Akweti’ amesema askari
polisi wanne walibughudhiwa na mashabiki na walipofyatua mabomu ya
machozi ndipo mashabiki hao wakaanza kukimbia na kukanyagana hali
iliyopelekea kusababisha vifo.
Aliongezea kwa kusema kuwa watu hao 15 wamekufa kwa kukosa hewa na wengine zaidi ya 24 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
MASHABIKI 15 WAFARIKI DUNIA KWENYE MECHI YA TP MAZEMBE NA AS VITA NCHINI CONGO
Reviewed by crispaseve
on
06:40
Rating:


Post a Comment