KUNDI LA BOKO HARAM WAONYESHA WASICHANA WALIOWATEKA
Kiongozi
wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru
wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo
wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo,
amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne
zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake mia moja wakiwa
wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni
wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo kutoka katika shule yao mjini
Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
Wakati huohuo Waziri wa mambo ya ndani nchini Nigeria amesema
serikali haitakubali masharti ya kundi la Boko Haram kwamba kwanza
liwaachilie wapiganaji wake kabla ya wasichana zaidi ya miambili
waliotekwa nyara waachiliwe.
Waziri Abba Moro amsema ni jambo la kipuuzi sana kwa kundi la kigaidi kujaribu kuweka masharti kama hayo.
Wasichana watatu kati ya waliooyeshwa na kuongea katika kanda
hiyo walikuwa wanavalia hijabu. Mmoja alisema kuwa amesilimu wakati
mwingine akisema yeye tayari ni Muisilamu.
KUNDI LA BOKO HARAM WAONYESHA WASICHANA WALIOWATEKA
Reviewed by crispaseve
on
06:42
Rating:

Post a Comment