Milipuko miwili yatokea,Gikomba, Nairobi
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba milipuko miwili imetokea karibu na Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi.
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na kuna hofu ya wanne kupoteza maisha yao kufikia sasa.
Milipuko ya leo imetokea siku moja baada ya
Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao
kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa
mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Milipuko miwili yatokea,Gikomba, Nairobi
Reviewed by crispaseve
on
05:48
Rating:
Post a Comment