MMILIKI WA LOS ANGELS CLIPPERS ‘DONALD STERLING AWAOMBA RADHI MASHABIKI
Mmiliki wa klabu ya mpira wa kikapu ya Los Angels Clippers
‘Donald Sterling’ ameomba radhi mashabiki kwa matamshi yake ya kibaguzi
aliyomtolea mpenzi wake.
Shirikisho la mchezo huo nchini Marekani lilimpiga marufuku
mmiliki huyo ya kutohudhuria mazoezi ya Clippers pamoja na mechi zake
sambamba na kutohusika katika maamuzi yoyote ya ndani ya timu hiyo ikiwa
na kulimwa faini ya dola za kimarekani milioni 2.8.
Hata hivyo Sterling alikiambia kituo cha televisheni cha
America Tv ya kwamba alifanya kosa kubwa sana ambalo hata hajui
anavyoweza kulirekebisha .
Kauli hiyo inakuwa ni ya kwanza kutolewa na Sterling tangu
kutokea kwa sakata hilo ambapo alikuwa akimkaripia mpenzi wake kwa
kumtaka kutojihusisha na watu weusi.
MMILIKI WA LOS ANGELS CLIPPERS ‘DONALD STERLING AWAOMBA RADHI MASHABIKI
Reviewed by crispaseve
on
06:55
Rating:
Post a Comment