SHAVU LINGINE LANUKIA KWA RYAN GIGGS NDANI YA UNITED
Mchezaji
mkongwe wa klabu ya Manchester United ‘Ryan Giggs’ huenda akapata shavu
la kuendelea kubaki katika benchi la ufundi kikosini hapo, baada ya
kocha anayetarajia kujiunga na mashetani hao wekundu ‘Louis Van Gaal’
kuweka wazi kuwa anapenda kumuacha kocha mmoja aliyekuwa katika kikosi
chake kipya kabla ya kujiunga na kuanza kazi rasmi.
Kocha huyo wa muda wa United hapo jana alishuhudia timu yake
hiyo ikienda sare ya bao moja kwa moja na Southampton katika mchezo
uliochezwa kwenye dimba la St.Marys
Stadium huku idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka wakisubiria
kuona uamuzi atakaotoa kocha huyo mdachi kuhusu hatma ya Giggs mara
atakapodhibitishwa kuwa kocha wa United baadae wiki hii .
‘’Napojiunga na klabu mpya mara zote huwa nambakisha kocha mmoja
kutoka benchi lililokuwepo, nikiwa Bayern nilimbakisha ‘Hermann
Gerland’ ambaye sasa anafanya kazi na Pep Guardiolla’’ alisema Van Gaal ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi.
SHAVU LINGINE LANUKIA KWA RYAN GIGGS NDANI YA UNITED
Reviewed by crispaseve
on
06:53
Rating:

Post a Comment