WAMBURA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA KITI CHA URAIS SIMBA SC
Wanachama
wa klabu ya wekundi wa msimbazi Simba wameendelea kumiminika kwenye
makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar
es salaam kwa ajili ya kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi
mbalimbali za Uongozi kupitia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Juni 29
mwaka huu.
Huku aliyewahi kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo na shirikisho
la soka Tanzania ‘Michael Richard Wambura’ kujitokeza kuchukua fomu ya
kuwania nafasi ya urais ambayo pia inawaniwa na Evans Kaveva na Andrew
Tupa baada ya kukamilisha zoezi hilo wanachama wanaomuunga mkono Wambura
waliweza kumuombea dua mgombea wao.
‘’Kuchukua kwangu fomu leo ni katika harakati za kuhitimisha
miaka 78 ya Simba kuendelea kutegemea watu fedha za mfukoni,
tunahitimisha mfumo ambao hauupeleki klabu ya Simba kujitawala kwa
misingi ya kiuchumi, kwa misingi ya kimashindano, wote tunaona na wote
tumeona kwa kipindi kirefu jinsi klabu yetu ilivyo’’ alisema Wambura.
Baada ya Wambura, ulifuata msafara wa Evans Aveva ambaye
amerudisha fomu aliyochukua jana ya kuwania urais ambapo msafara wake
umeongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali ulioanzia
mtaa wa Lumumba na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wa timu hiyo
waliokuwa wamefurika nje ya jengo makao makuu ya klabu hiyo na kisha
alifuata mgombea wa nafasi ya umakamu wa Rais Bwana Swedi Mkwabi.
WAMBURA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA KITI CHA URAIS SIMBA SC
Reviewed by crispaseve
on
06:52
Rating:
Post a Comment