WAHAMIAJI 36 WAFA MAJI NA WENGINE 52 WAOKOLEWA KATIKA PWANI YA LIBYA
Wahamiaji 36 wamekufa maji na wengine 52 wameokolewa baada ya
boti yao kuzama katika pwani ya Libya ambayo inasemekana kuwa njia kuu
ya wahamiaji wengi wanaojaribu kwenda Ulaya.
Mbali na wahamiaji waliokufa na kuokolewa, kuna wengine 54
ambao bado hawajaonekana baada ya wahamiaji walionusurika kusema kuwa
boti ilikuwa na zaidi ya watu 130.
Mwishoni mwa wiki waziri wa Libya wa mambo ya ndani aliomba
umoja wa Ulaya kufanya juhudi zaidi za kusaidia kupunguza wimbi la
wahamiaji wanaopjaribu kwenda Ulaya kutafuta Maisha.
WAHAMIAJI 36 WAFA MAJI NA WENGINE 52 WAOKOLEWA KATIKA PWANI YA LIBYA
Reviewed by crispaseve
on
06:45
Rating:


Post a Comment