ZIARA YA MWENGE WA UHURU WILAYANI KALAMBO MKOANI RUKWA LEO
Katibu Tawala wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Festo Chonya wa pili kulia akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian mara baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nkasi mapema leo asubuhi tarehe 22 Mei, 2014.
Mratibu wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu Abuubakar Serungwe kulia akitoa neno la shukurani kwa uongozi wa Wilaya ya Nkasi kwa ushirikiano walioutoa wakati Mwenge huo upo Wilayani humo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bi. Rachel Kassanda akizindua rasmi wodi ya wazazi ya Samazi mwambao wa Ziwa Tanganyika Wilayani Kalambo leo tarehe 22 Mei, 2014. Kulia anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Kimanta akitoa maelezo mafupi kuhusu kitanda cha kujifunguliza wazazi kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bi. Rachel Kassanda baada kuzindua wodi hiyo ya wazazi ya Samazi mwambao mwa ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa.
Sehemu ya wananchi wengi wa Kijiji cha Samazi mwambao mwa ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa walikusanyika kushuhudia ujio wa Mwenge wa Uhuru kijijini hapo.
Kwa wale waliokosa pa kukaa walilazimika kupanda miti na kuhatarisha maisha yao ili wapate fursa ya kupata taswira iliyo mwanana ya Mwenge wa Uhuru.
Ndugu Enock Nguvumali Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji Nyuki Kijiji cha Kisumba akishika Mwenge wa Uhuru leo tarehe 22 Mei, 2014. Mapema kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bi. Rachel Kassanda alizindua mradi wa kutundika mizinga ya kisasa ya nyuki katika Kijiji cha hicho.
Wadau wa Mwenge wa Uhuru ambao pia ni wakuu wa idara katika Wilaya Kalambo Ndugu Mirunga (kushoto) na Maholani wakijadili jambo muda mfupi kabla ya kusomwa Risala ya Utii ya Mwenge wa Uhuru kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani Kalambo.- Na Hamza Temba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com
ZIARA YA MWENGE WA UHURU WILAYANI KALAMBO MKOANI RUKWA LEO
Reviewed by crispaseve
on
00:37
Rating:
Post a Comment