MILLEN MAGESE AOMBA USHIRIKIANO SERIKALINI NA WANANCHI KWA UJUMLA
MWANAMITINDO wa kimataifa wa hapa nchini na Miss
Tanzania 2001 anaefanya kazi yake hiyo nchini Marekani Millen Magese ameiomba
serikali kumpatia eneo ambalo atalitumia kujenga hospitali maalum ya
kushugulikia afya ya wanawake.
Millen alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza
na watu mbalimbali waliohudhuria semina ya bure kuhusiana na hali ya Endometriosis
inayowakabili wanawake wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla. Millen anakabiliwa na tatizo hilo la
Endometriosis ambalo ni hali ya mwanamke kushindwa kupata siku zake za mwezi
katika hali ya kawaida na yenye kuleta madhara kwa afya yake hususan kwenye
uzazi.
Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamke maarufu
na mwenye ushawishi katika jamii yake ameamua kutoa elimu ya tatizo hilo ili
kusaidia kuongeza uwelewa wa suala hilo ili kuwasaidia wanawake wengine.
Alisema kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiana na afya
hivyo linahitaji msaada wa ukaribu zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya kwa ajili
ya kusaidia wasichana na wanawake wenye matatizo mengine ya kiafya pia. Alisema kuwa mwanamke anaekabiliwa na tatizo
kama hilo anafikia wakati anakuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji na lakini
kutokana na ugeni wa tatizo husika kwa hapa nchini hakuna vifaa vya kutambua na
kufanyia upasuaji huo. Ambapo mpaka sasa ni KCMC pekee ndio wana kifaa cha
kuweza kutambua tatizo hilo.
Alisema kuwa ameshaanza kupata misaada kutoka
kwa watu mbalimbali wa Marekani kama vile taasisi ya Swan Development LLC, Texas
ambao wameahidi kumpatia mashine za za kutambua tatizo na upasuaji pamoja na dawa,
ambapo angependa ziwekwe hospital ya Dar es salaam kulingana na mapendekezo ya
wadau ingawa lengo lake la muda mrefu ni kufungua hospital itakayojihusisha na
magonjwa ya wanawake na ndio maana anaomba msaada wa serikali na wananchi kwa
ujumla ili kufanikisha lengo hilo.
"Ningependa kama kufungua hiyo hospitali
basi iwe ni Dodoma au Bagamoyo kwa kuwa ni rahisi zaidi kwa Dodoma watu
mbalimbali kufika na kwa Bagamoyo inakuwa ni rahisi pia kuzifikisha mashine
kutoka Bandarini"alisema Millen. Aliongeza kuwa kwa kuwa tatizo hilo linakuja
kutokana na kushindwa kulishughulikia mapema hasa wakati msichana anapokuwa
amevunja ungo na kuanza siku zake za hezi akiwa na maumivu makali.
Aliwataka watoto kuwaambia wazazi pindi
wanapokuwa wakipatwa na maumivu makali yaliyopitiliza wakati wakiwa kwenye siku
zao za hezi na pia wazazi kujadiliana na watoto wao punde hali hiyo inapotokea
na kuwawahisha hospital ili wapatiwe huduma sahihi.
Katika tukio
hilo la jana Millen aliambatana na madaktari bingwa wa wanawake wawili ambao ni
daktari Fadhlun M. Alwy na daktari Belinda Ballandya wote kutoka chuo kikuu cha
Afya Muhimbili ambao walitoa elimu ihusianayo na tatizo hilo na Endometriosis.
Watu wengi walijitokeza kupata somo hilo na
kuzungumzia suala hilo wakiwemo, wanawake, wananume na watoto.
MILLEN MAGESE AOMBA USHIRIKIANO SERIKALINI NA WANANCHI KWA UJUMLA
Reviewed by crispaseve
on
10:16
Rating:
Post a Comment