WANENGUAJI WA KHANGA MOKO WAJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI
Wakata
nyonga maarufu wa kundi la ‘Khanga Moko Laki Si Pesa’ wamenusurika
kupoteza maisha baada ya mtu mmoja kudaiwa kuwashambulia kwa risasi,
hali iliyopelekea wasamaria wema kuwakimbiza katika hospitali ya
Mwananyamala kwa ajili ya kunusuru maisha yao.
Tukio hilo linaelezwa kutokea wakati wanenguaji hao, Zawia
pamoja na mwenzake wakisasambua kwa matarumbeta kwenye harusi kabla ya
kufyatuliwa risasi zilizowajeruhi eneo la pajani na mwingine kwenye
makalio. Hali za wagonjwa zinatajwa kuimarika licha ya kulazimika
kuendelea kukaa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi.

Picha na Geah Habib Wa HekaHeka
WANENGUAJI WA KHANGA MOKO WAJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI
Reviewed by crispaseve
on
13:32
Rating:
Post a Comment