WAZIRI HAWA GHASIA AZINDUA KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM
Mtendaji
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Henry Mambo akiwakaribisha washiriki
pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia(huyumo
katika picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano la miaka 50 ya muungano katika utumishi
wa umma ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere katika leo, jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akisoma
risala ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.
Hawa Ghasia (hayumo katika picha), wakati wa ufunguzi wa kongamano la miaka 50 ya
Muungano katika utumishi wa umma, katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini
Dar es Salaam, leo .
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa
Ghasia akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kongamano la Miaka 50 ya Muungano
katika Utumishi wa Umma,katika ukumbi wa
kimataifa wa Mwl. Nyerere leo jijini Dar es Salaam, kongamano hilo la siku
mbili linaambatana na maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi
Mmoja.
Watumishi
wa umma na washiriki wa Kongamano la
Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma wakimfuatilia kwa makini mgeni
rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Hawa Ghasia (hayumo katika
picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl.
Nyerere leo, jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia (katikati), akiwa
katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Miaka 50 katika Utumishi wa Umma baada ya kufungua rasmi
kongamano hilo la siku mbili Juni 19 na 20 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl.
Nyerere, jijini Dar es Salaam. Lengo la kongamano ni kujadili maada mbalimbali
zinazohusu utumishi wa umma. (Picha na Lorietha Laurence).
========= ======== =======
Na Ismail
Ngayonga
Maelezo
Dar es
Salaam
19. Juni,
2014
SERIKALI imewataka wananchi
kuzingatia taratibu za kimsingi
zinazopaswa kufuatwa na mteja wakati wa ufuatiaji na utoaji wa huduma
mbalimbali zinazotolewa na watoa huduma katika sekta ya Utumishi wa Umma nchini.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe (19.
Juni, 2014) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia wakati alipokuwa akifungua kongamano la Wiki ya
Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam. Waziri Ghasia alisema katika utoaji
wa huduma za umma, mwananchi ambaye ndiye mteja mkuu katika utumishi wa umma
ana wajibu wa kuwasilisha taarifa muhimu zitakazoombwa na mtoa huduma wa sekta
ya umma, na mwananchi atapaswa kuziwasilisha kama sehemu ya udhibitisho wa kutolewa
kwa huduma husika.
“Kwa mfano mwananchi anayehitaji
huduma ya cheti cha kuzaliwa kwa mtoto wake atapaswa kuwasilisha kadi ya
hospitali, ambayo itaombwa na mhudumu wa afya, hivyo ni wajibu wa wananchi
kutimiza kigezo hicho kama sharti la msingi la kupatiwa huduma hiyo” alisema
Waziri Ghasia.
Akifafanua zaidi alisema ni dhahiri
zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya umma na zipo zinazofanyiwa
kazi na baadhi yake zinazohitaji ushirikishwaji wa wadau na kwa kulitambua
suala hilo Serikali iliandaa kongamano hilo
ili kuisaidia kutekeleza mipango yake kwa ufanisi kupitia Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa.
Aidha Waziri Ghasia alisema katika
kipindi cha miaka 50 ya utumishi wa Muungano, Serikali imechukua hatua
mbalimbali za kuimarisha sekta ya utumishi wa umma ikiwemo ubunifu wa Sera
mbalimbali zinazotekelezwa kupitia kamati za mashauriano baina ya pande mbili
za Muungano.
Waziri Ghasia aliongeza kuwa zipo
changamoto mbalimbali za kimaendeleo zinazolikabili taifa, ambapo kwa kiasi
kikubwa utatuzi wake unategemea namna sekta ya utumishi wa umma ilivyojipanga
na kutekeleza wajibu wake.
“Sekta binafsi, Asasi za Kiraia na
Sekta isiyo rasmi ni sekta muhimu kwa maendeleo ya Taifa kuweza kukaa pamoja na
kubadilishana mawazo na uzoefu katika maeneo yetu, na zote kwa pamoja zina
mchango mkubwa kwa kuwa zinasaidia kuwasilisha mawazo ya jamii Serikalini”
alisema Waziri Ghasia.
Aliongeza kuwa mwaka 2011 Serikali
ilibuni sera ya ushirikiano baina yake na sekta binafsi yaani Private
Partnership Policy iliyopitishwa mwaka 2010 na kufuatiwa na sheria ya
kutekeleza sera hiyo na kwa upande wa Asasi za kiraia upo mwongozo wa
kushirikiana na asasi hizo uliotolewa mwaka 2012.
Akizungumzia suala la maadili katika
utumishi wa Umma, Waziri Ghasia alisema wapo baadhi ya watumishi wanaokiuka
maadili ya kazi ingawa si wote, kwani kwa sasa Serikali inatafakari changamoto
na mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka 50 ya utumishi
wa Umma nchini.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu alisema maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni maonesho ya wazi na yanahudhuriwa na wananchi
wote yanayotoa fursa kwa watoa huduma a,bao ni taasisi za umma kukutana moja
kwa moja na wateja na wananchi kwa upande mwingine.
WAZIRI HAWA GHASIA AZINDUA KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
11:52
Rating:

Post a Comment