Header AD

MFUMUKO WA BEI NCHINI UMEPUNGUA - OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU.

 Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kupungua kwa  mfumuko wa bei nchini.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini  kwa mwezi Juni 2014 umepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma za jamii katika maeneo mbalimbali.
 
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2014 umepungua na kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.5.
 
Amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi Juni 2014 imepungua ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Mei kutokana na hali ya kupungua kwa bei  kwenye  bidhaa na huduma
 
 Ameeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Juni umeongezeka hadi asilimia 8.5 kutoka asilimia 7.9 za mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi imeongezeka hadi asilimia 7.8 kutoka asilimia 7.2 za mwezi uliopita huku badiliko la fahirisi za bidhaa zisizo za vyakula likipungua hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Aprili 2014 kutoka asilimia 7.2 iliyokuwepo mwezi uliopita.
MFUMUKO WA BEI NCHINI UMEPUNGUA - OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU. MFUMUKO WA BEI NCHINI UMEPUNGUA - OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU. Reviewed by crispaseve on 09:27 Rating: 5

No comments

Post AD