NOOIJ ASEMA STARS IPO TAYARI KUUA MAMBA JUMAPILI, CANNAVARO AAHIDI WATALIPA KISASA CHA KUNYANYASWA NA MSUMBIJI
KOCHA
Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart
Nooij amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumapili
dhidi ya Msumbiji hatua za awali Kombe la Mataifa ya Afika (AFCON).
Nooij
ambaye amewahi kuifundisha Msumbiji amesema katika Mkutano na Waandishi
wa Habari hoteli ya Coutyard, eneo la Sea View, Dar es Salaam kwamba
wachezaji wake wote wapo fiti kwa mchezo huo.
“Nafahamu
sana mchezo utakuwa mgumu, hii ni timu yangu na timu yenu pia, naamini
mshindi ni yule ambaye atacheza kitimu zaidi Jumapili,”amesema.
Amesikitika
kiungo Jonas Mkude ameshindwa kuhusika na mchezo wa Jumapili kutokana
na kusumbuliwa na maumivu ya goti, hata hivyo amesema ana matumaini m
mchezaji huyo wa Simba anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Ametaja
kikosi alichoteua kwa ajili ya mchezo wa kesho, kuwa ni makipa Deo
Munishi ‘Dida’ na Aishi Manula, mabeki Said Mourad, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Aggrey Morris, Kevin Yondan na Edward Charles, wakati
viungo ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Shaaban Nditi, Simon Msuva,
Himid Mao, Mwinyi Kazimoto, Khamis Mcha, Ramadhani Singano ‘Messi’,
Haroun Chanongo, Amri Kiemba na washambuliaji Mrisho Ngassa, Thomas
Ulimwengu, Mbwana Samatta na John Bocco,
Kwa
upande wake, Nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema
kwamba anaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi Uwanja wa taifa mjini Dar
es Salaam kuisapoti timu yao.
“Tunashukuru
hadi kufika hapa, ni matunda ya kupambana kwa juhudi na pia sapoti
yenu, kwa hivyo tunaomba muendelee kuwa nasi Jumapili, watu waje kwa
wingi wasapoti timu, ifanya vizuri,”amesema Cannavaro.Aidha nahodha huyo
wa taifa Stars amesema bado ana kumbukumbu za kipigo walichokipata
dhidi ya Msumbiji mwaka 2007,wakati Nooij akiwa kocha mkuu wa Mambas,
na kwa maana hiyo hivi sasa akiwa chini yake atafanya kila juhudi kwa
faida ya Watanzania na yeye mwenyewe binafsi.
Stars
itamenyana na Msumbiji Jumapili katika mchezo wa kwanza wa hatua ya
mwisho wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya
AFCON mwakani nchini Morocco, ambao kiingilio cha chini kitakuwa Sh.
7,000.
Stars
ilifika hatua hii baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2,
ikishinda 1-0 Dar es Salaam na kwenda kulazimisha sare ya 2-2 Harare.
Timu
itakayofuzu hatua hii itaingia kwenye Kundi C ambalo lina timu za
Zambia, Cerpe Verde na Niger zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo,
kuwania tiketi ya Morocco mwakani.
Katika
kuwania tiketi ya AFCON ya mwaka jana nchini Afrika Kusini, Tanzania
ilitolewa na Msumbiji kwa penalti 5-4 baada ya sare ya jumla ya 2-2 Dar
es Salaam na Maputo, Stars ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen.
Stars
inaonekana kuwa na maandalizi mazuri safari hii chini Mholanzi, Nooi na
uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais Jamal
Malinzi.
Baada
ya kuitoa Zimbabwe, wachezaji walipata mapumziko ya wiki moja, kabla ya
kwenda Botswana kuweka kambi ya wiki, na waliporejea Mbeya kuweka kambi
ya wiki moja na ushei.
Nchini Botswana, pamoja na mazoezi, pia Stars ilipata mechi tatu za kujipima nguvu, ambazo
walifungwa
mbili, moja dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Botswana mabao 4-2 na
nyingine dhidi ya timu ya jeshi la nchini humo, BDF walishinda moja 3-1
na kufungwa moja 2-1.
Tanzania
imewahi kushiriki mara moja tu AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria ambako
ilitolewa katika hatua ya makundi, ilipokuwa pamoja na wenyeji Nigeria,
Ivory Coast na Misri, Kundi A. Ilifungwa 3-0 na Nigeria, 2-1 na Misri na
kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast.
![]() |
Kocha Mart Nooij kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Kulia Msaidizi wake, Salum Mayanga |
![]() |
Kutoka kulia Shomary Kapombe, Mbwana Samatta na Cannavaro |
![]() |
Kutoka kulia Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto |
NOOIJ ASEMA STARS IPO TAYARI KUUA MAMBA JUMAPILI, CANNAVARO AAHIDI WATALIPA KISASA CHA KUNYANYASWA NA MSUMBIJI
Reviewed by crispaseve
on
08:54
Rating:

Post a Comment