YULE MFUNGWA HENDSAMU BOI AULIWA NA MKEWE MASAA MACHACHE BAADA YA KUACHIWA HURU

Uchunguzi wa polisi umesema kwamba Meek aliachiwa huru usiku wa Jumanne(Julai 14) na
kwenda nyumbani kwa mama yake ambapo usiku wa kuamkia Jumatano mwili
wake ulikutwa umelala chini ya barabara ukiwa umejeruhiwa na kitu
kinachodhaniwa ni risasi au kisu kwa kile kilichotajwa kuwa ni ugomvi
uliotokea baina yake na mkewe aitwaye Lashada.
Polisi imefanikiwa kumkamata Lashanda Meek pamoja na
ushahidi wa bastola na gari dogo alilotumia kukimbia nalo eneo la tukio
kwenye nyumba aliyokuwa amejificha.
Mkuu wa polisi wa Stockton, Tom Morris, amesema kwa sasa
Lashada anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya mkoa na baada ya hapo
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
YULE MFUNGWA HENDSAMU BOI AULIWA NA MKEWE MASAA MACHACHE BAADA YA KUACHIWA HURU
Reviewed by crispaseve
on
08:43
Rating:
Post a Comment