TFF yaitaka Airtel kudhamini U-20
Meneja
Masoko wa Airtel Tanzania Rebeca Mauma akizungumza wakati wa semina
elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya washiriki wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars wakifutilia kwa
makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo iliyofanyika
uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu
mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisisitiza jambo wakati wa semina
elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiteta na Katibu Mkuu wa
TFF Selestine Mwesigwa wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars
iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi na Mwenyekiti wa DRFA Almasi
Kasongo.
========== -========== -========
Katibu
Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Selestine Mwesigwa
amesisitiza umuhimu wa programu za vijana kwa maendeleo ya soka nchini
na kuitaka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuangalia
uwezekano wa kuwa wadhamini wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 20.
Akifungua
semina elekezi kwa makatibu wakuu wa mikoa inayoshiriki mashindano ya
vijana ya Airtel Rising Stars (ARS) iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam Jumamosi Julai 19, 2014 Mwesigwa alisema hali halisi
inaonyesha kwamba miaka michache ijayo wachezaji wengi watakaounda timu
ya taifa ya U-20 watatokana na ARS hivyo ni vema kampuni ya Airtel ikawa
mdhamini mkuu wa timu hiyo.
Alisema
kuwa suala la programu za vijana ni agenda namba moja ya TFF na
kuzitaka timu za ligi kuu kuzingatia maagizo ya shirikisho hilo la kuwa
na timu za vijana. “Klabu ya Simba imefanikiwa sana katika suala hili na
ni vema timu nyingine za ligi kuu zikaiga mfano huo”, alisema Mwesigwa
na kuipongeza Airtel kwa kuwekeza katika soka la vijana.
“Wachezaji
wanapolelewa na klabu tangu wakiwa wadogo inakuwa ni rahisi kwao
kuendana na maadili ya klabu hiyvo kuwa na wachezaji wenye nidhamu ya
hali ya juu tofauti na wachezaji waosajiliwa kutoka sehemu mbali mbali
wakiwa na umri mkubwa”, alisema.
Aliwataka
makatibu hao wa mikoa kuzingatia kanuni ikiwa ni pamoja na umri ili
kuwafanya vijana watakaoshiriki mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa
na ushindani ulio sawa. Mashindano ya ARS yanashirikisha vijana chini ya
umri wa miaka 17.
Mwesigwa
aliungwa mkono na Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi
aliyesema kuwa programu za vijana e.g. ARS ndiyo mkombozi wa kweli wa
soka popete pale duniani.
Mashindano
hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa Julai 27 na
kushirikisha mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ilala, Kinondoni na
Temeke kwa upande wa wavulana huku timu za wasichana zikitoka mikoa ya
Mwanza, Mbeya, Zanzibar, Ilala, Kinondoni na Temeke.
Akiongea
katika semina hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando
aliwapongeza viongozi wa mikoa kwa kazi nzuri iliyoiwezesha Tanzania
kutwaa ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya ARS (wasichana)
yaliyofanyika Nigeria na kuzawadiwa USD 10,000, medali na vikombe.
“Vile
vile timu ya wavulana ilifanya vizuri sana na ni imani yangu kwamba
mwaka huu Tanzania itashinda vikombe kwa wasichana na wavulana”, alisema
na kusisitiza nia thabiti ya Airtel kuendelea kuboresha mashindano
hayo.
Naye
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi aliwataka makatibu hao
kufanyakazi kwa karibu na kamati ya vijana ya TFF inayosimamia
mashindano hayo.
TFF yaitaka Airtel kudhamini U-20
Reviewed by crispaseve
on
02:23
Rating:
Post a Comment