Header AD

CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA


Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa  uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiwaongoza wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda (katikati)  akizungumza  jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Mathew Luhanga (kushoto).Wengine Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam wakiendelea na shughuli mbalimbali chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiwakaribisha  wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali  na Wanajumuiya wa Chuo Cha Elimu ya Biashara wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Polisi kikiongozwa na Afande Juma Boha Mnyaa kikitoa burudani ya ngoma ya asili ya ya Kibati kutoka Kusini Pemba wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es salaam.
CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA Reviewed by crispaseve on 09:24 Rating: 5

No comments

Post AD