Header AD

UGANDA YAFUTA SHERIA DHIDI YA USHOGA

Taswira za waliokuwa wakipinga sheria dhidi ya ushoga nchini Uganda.
MAHAKAMA ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.
Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana siyo tu Uganda bali duniani kote ambapo mataifa ya magharibi yalilazimika kuingilia kati.
Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada hivyo ni kinyume na sheria.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa nchini Uganda, lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.
Mataifa kadhaa ya magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.
Chanzo: BBCSWAHILI
UGANDA YAFUTA SHERIA DHIDI YA USHOGA UGANDA YAFUTA SHERIA DHIDI YA USHOGA Reviewed by crispaseve on 09:23 Rating: 5

No comments

Post AD