Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar

Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia mbele) na
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto mbele),
wakiwaongoza wafanyakazi wa Airtel Tanzania na wanafunzi kwenye
matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi
milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu ,
yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel , Barabara ya Ali Hassan
Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41,
jijini Dar es Salaam jana.

Wafanyakazi
wa Tanzania na wanafunzi wakiwa kwenye matembezi ya hisani yenye lengo
la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya
kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika
Makao Makuu ya Airtel, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo,
Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam
jana.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akimkabidhi
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani, funguo za kisima kipya cha
maji safi kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na
Wafanyakazi wake, katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla
iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana.
Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano
Malya (kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu
kushoto), na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Mwemba Mwilima.

Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Benedict Missani (kulia) akifungua ili kukagua kisima
kipya cha maji safi kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana
na Wafanyakazi wake, katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, baada ya
kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil
Colaso (wa pili kushoto), wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo
la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto) na Mwalimu Mkuu
wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto).

Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akifungulia maji ya bomba
kama ishara ya uzinduzi rasmi wa kisima kipya cha maji safi
kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi
wake, katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika
shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia
ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto) na Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa nne kushoto).
Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar
Reviewed by crispaseve
on
06:05
Rating:

Post a Comment