DIAMOND PLATNUMZ, MZEE YUSUF WAAHIDI KUANGUSHA SHOO YA KUFA MTU DAR LIVE SIKUKUU YA X-MAS
WASANII
mahiri nchini Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' na Mzee Yusuf wamewaahidi
mashabiki wa burudani hususani wa Jiji la Dar es Salaam kutokosa kesho
katika Ukumbi wa Dar Live kushuhudia shoo ya kibabe inayotambulika kama Tamasha la Wafalme.
Wakiongea
na wanahabari katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd zilizopo
Mwenge-Bamaga jijini Dar, wakali hao wamesema wamejiandaa vilivyo kwa
ajili ya shoo hiyo itakayoacha historia katika pande za Mbagala-Zakhem,
jijini Dar.
Naye
Meneja wa Dar Live, Abdallah Mrisho amewataka mashabiki wa burudani
kuhudhuria kwa wingi kesho katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live
maana kila kitu kiko safi kuanzia ulinzi na huduma zote muhimu.
Shoo
hiyo ya aina yake itaanza asubuhi kwa burudani za watoto ambapo kundi
la sarakasi la Masai Worriors litahakikisha linatoa burudani ya nguvu
kwa watoto wote kwa kuwapa staili mbalimbali za sarakasi na
mazingaombwe. Pia watoto wataburudika na michezo kibao kama vile
kuogelea, kubembea, kuteleza huku kila mmoja atakayehudhuria kurudi na
zawadi kemkem nyumbani kwao. Kiingilio cha Tamasha la Wafalme kitakuwa
shilingi 10,000 kawaida wakati kwa VIP kiingilio kikiwa shilingi 20,000.
WOTE MNAKARIBISHWA!
DIAMOND PLATNUMZ, MZEE YUSUF WAAHIDI KUANGUSHA SHOO YA KUFA MTU DAR LIVE SIKUKUU YA X-MAS
Reviewed by crispaseve
on
11:44
Rating:
Post a Comment