KOCHA SUPER D AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA VIFAA
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akimkabidhi vifaa
bondia Mussa Chitepete wa Songea vilivyotolewa na Super D kwa
kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wengine kulia ni Kiliani
Shayo na Rajabu Mkamba ambaye ni mdau mkubwa wa kuhamasisha kusaidia
mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kushilikiana na marafiki
zake wa kwenye mtandao wa kijamii wa watsupp wamemkabidhi vifaa bondia
Mussa Chitepete wa Songea kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumwi
nchini
Super D alimkabidhi vifaa hivyo bondia
huyo hivi karibuni alivyotembelea jijini Dar es salaam kuja kushiliki
mchezo wa masumbwi ambapo alipatiwa glove,gum shit,clip bandeji pamoja
na kamba kwa ajili ya kurukia
vifaa hivyo vilivyotolewa na super D
kwa kushilikiana na mdau mkubwa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mkumba ambaye ndie mwamasishaji mkubwa katika mtandao huo kwa ajili ya
kusaidia mabondia
baada ya kukabidhiwa msaada huo bondia Mussa Chitepete wa Songea alishukulu wadau mbalimbali kwa kumpatia vifaa na
kumpongeza kocha Super D kwa kuanzisha mtandao ambaoumekuwa muhimu sana
kwangu kwa mimi kupata vifaa najua sitotumia peke yangu wapo na wenzangu
tutakao tumia nao pamoja vifaa hivi ambavyo itakuwa chachu ya kuinua
mchezo wa masumbwi Songea
KOCHA SUPER D AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA VIFAA
Reviewed by crispaseve
on
11:28
Rating:
Post a Comment