FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA

Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni
ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo
jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na
kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na
kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya
nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi yanayofanyika kuombea taifa la
Tanzania yapokelewa na Mungu , Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani
Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha
mungu kwa njia ya uimbaji 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua
albam ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya
yenye inayoitwa Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama. 

Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya huku Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki katika maombi hayo. 

Mwimbaji
wa muziki wa injili Upendo Nkone akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya wakati wa tamasha la Krismas leo. 

Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa jukwaani.
FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA
Reviewed by crispaseve
on
11:51
Rating:
Post a Comment