Mawazo 50, kuanzisha blogu & tovuti ya Kipekee
Hivi sasa kumiliki blogu au tovuti ni jambo jepesi na la kawaida sana.
Ni tofauti kabisa na miaka ya nyuma kidogo, kipindi ambacho watumiaji
wa mtandao wa internet walikuwa wachache sana. Lakini zaidi, ni unafuu
wa utengenezaji na ubunifu wa blogu hizo na tovuti (Gharama zipo nyingi
tu…).
Lakini kama unataka kuwa na blogu au tovuti ama umewahi kuwa wazo hilo
lakini kwa sababu mbalimbali ukashindwa kutimiza na kuanzisha blogu au
tovuti yak, leo ninataka nikuoneshe mawazo 50 ya kuanzisha blogu na
tovuti ya kipekee.
Zipo blogu nyingi sana duniani, hapa kwetu +255, Tanzania zimejaa tele.
Lakini wengi wamekuwa wakitaka blogu za aina moja, hasa blogu na tovuti
za udaku, habari na burudani hususani michezo na suala zima la muziki.
Imefikia hatua watu wengine wanadhani blogu ni kwa ajili ya udaku na
muziki tu. Kuwa tofauti kuna changamoto zake, lakini hakika mwisho wa
siku utofauti wako utakuja kuleta mabadiliko makubwa sana, Usiogope kuwa
tofauti, Usiogope kuanzisha jambo jipya katika msitu wa aina moja ya
wazo, anzisha wazo lako,lipambe, liweke katika viwango vizuri kisha ona
mafanikio.
Yafuatayo sasa ni mawazo 50 ya kuanzisha blogu au tovuti ya kipekee,
upekee huu sio kwamba ni wewe pekeyako, Coca-cola na Pepsi wanatengeneza
vinywaji lakini wote wamefanikiwa na yupo mmoja mbabe zaidi.
#50. Ushauri na mipango ya maisha kwa Vijana.
#49. Jinsi ya kupanga na kujenga nyumba ya ndoto zako.
#48. Mapishi.
#47. Afya na Lishe.
#46. Tahakiki na uchambuzi wa vitabu mbalimbali.
#45. Ujasiriamali.
#44. Ajira kwa wasiokuwa na elimu ngazi za juu sana.
#43. Uchunguzi wa Makabila ya kiasili.
#42. Hadithi za Kale.
#41. Maisha ya Kisasa.
#40. Fasheni.
#39. Mikutano mtandaoni, kwa video.
#38. Utalii.
#37. Mafunzo ya moja kwa moja mtandaoni.
#36. Jinsi ya kutunza Magari na vyombo vingine vya moto.
#35. Neno la Mungu/Allah
#34. Kuandika CV na njia za kupata kazi.
#33. Jinsi ya kupiga picha na kurekodi video.
#32. Maisha ya watu maarufu.
#31. Jinsi ya Kuishi maisha rahisi bila kutumia pesa nyingi.
#30. Teknohama
#29. Mafunzo ya ufundi stadi.
#28. Sheria.
#27. Mafunzo ya Gitaa/Kinanda/Ngoma/Zumari/Malimba…n.k
#26. Michezo ya Bahati nasibu/ Betting.
#25. Tovuti/Blogu ya familia.
#24. Jinsi ya kuongea katika mihadhara na mawasilisho ya kibiashara.
#23. Maisha ya Shule/Chuo.
#22. (Picha nyingi-Habari fupi sana) za michezo tu.
#21. Jinsi ya kuwa maarufu.
#20. Magonjwa na Tiba asilia.
#19. Urembo na Mapambo.
#18. Ubunifu wa sebule, vyumba na Dining.
#17. Mafunzo ya kugha mf. Kiswahili, Kiingereza, Kichaga, Kiganda, Kikikuyu.
#16. Kilimo na Ufugaji.
#15. Jinsi ya kujitunza na kujilinda.
#14. Mipangilio na Matumizi ya Pesa.
#13. Masomo ya Computer.
#12. Marafiki.
#11. Siasa.
#10. Interview na watu wenye mafanikio. Mf. Bwana Shamba, Mtangazaji, Mwandishi wa Vitabu.
#9. Jinsi ya kujenga na kupunguza mwili.
#8. Mahusiano na Mawasiliano baina ya Jinsia ya Kiume na Kike.
#7. Malezi ya watoto wadogo na vichanga.
#6. Filamu za Kibongo.
#5. Mitindo na Sanaa za asili.
#4. Mandhari za kuvutia wilayani, mkoani au nchini mwako.
#3. Maisha katika jamii.
#2. Kutanisha wapenzi/ Mahusiano.
#1. Biashara na Njia za mawasilano.
Ni matumaini yangu kuwa baada ya kupitia mawazo yote hayo, umepata
mwanga wa nini blogu au tovuti yako ifanye. Kumbuka, mafanikio
hupatikana baada ya muda mrefu sana wa kujitolea muda wako kuhakikisha
malengo yako yanatimia. Hata hadithi zote za watu wenye mafaniko
duniani, wengi wamepitia misukosuko ambayo nusura ingefuta kabisa ndoto
zao. Ni vyema kama una uwezo wa kutengeneza blogu (maana ni bure..)
ujitengenezee, lakini pia unaweza kuwasiliana nami, pamoja tukatengeneza blogu au tovuti ya ndoto zako.
Kama imekuvutia, Tafadhali wajulishe pia marafiki, kupitia mitandao ya kijamii na usisite kutoa maoni au pia unaweza kutoa mawazo yako kuhusu kuanzisha blogu na tovuti.
Mawazo 50, kuanzisha blogu & tovuti ya Kipekee
Reviewed by crispaseve
on
15:12
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
15:12
Rating:


Post a Comment