ITV sasa kuonekana kupitia DStv

MultiChoice
Africa, kampuni inayoongoza katika kutoa burudani ya kulipiwa ya
dijitali pamoja na IPP Media wamesaini makubaliano yatakayoleta chaneli
maarufu zaidi Tanzania, ITV, kuwa sehemu ya jukwaa la DStv.
Ushirikiano
huu wa kusisimua utawapa watazamaji wa Tanzania kote nchini fursa ya
kuangalia vipindi vilivyotengenezwa hapa hapa nchini vikiwa na ubora
mkubwa kidijitali. Chaneli hii itapatikana kwenye vifurushi vyote vya
DStv ikiwemo kifurushi kilichozinduliwa hivi karibuni cha Bomba, Family,
Compact, Compact Plus na Premium.
Akizungumzia
ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV Bi Joyce Mhaville alisema:
“Tunajivunia sana ushirikiano huu ambao tumekuwa tukiufanyia kazi kwa
muda mrefu. Fursa zinazojitokeza kutokana na makubaliano haya
yatanufaisha kampuni zote mbili pamoja na kuwanufaisha watazamaji wetu,
hasa kwa wakati huu ambao tumehama kutoka katika mfumo wa analojia
kuingia dijitali. ITV ina vipindi vyenye ubora vilivyotengenezwa hapa
hapa nchini na ambavyo vinawafaa watanzania wakati DStv itatuwezesha
kupanua wigo wetu.”
Akizungumza
juu ya hili, Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kanda ya Afrika Mashariki
Bwn Stephen Isaboke alisema: “MultiChoice imejizatiti kuwapa watazamaji
wake chaneli nyingi mbalimbali zikiwepo zinazoonyesha vipindi vya hapa
hapa na vile vya nje.
Kwa
kuwa ITV inakuwa kwa kasi na ina watazamaji wengi, ushirikiano huu
utatufaa kwa vile unaongeza vipindi vilivyotengenezwa hapa nchini.
Tutaendelea kuwekeza katika kuwaletea vipindi vyenye utofauti. Kwa
kupitia vifurushi vyetu mbalimbali, tunawapa wateja wetu chaneli nyingi
kwa bei tofauti ili wawe na uwanja mpana wa kuchagua.”
ITV sasa kuonekana kupitia DStv
Reviewed by crispaseve
on
06:58
Rating:

Post a Comment