Jerry Muro Afisa Habari Mpya Wa Timu Ya Yanga

Afisa Habari mpya wa timu ya Yanga Jerry Muro
----
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Klabu ya Yanga ya
jijini Dar es Salaam imemtangaza rasmi Kocha Hans van Pluijm kuwa kocha
mkuu wa timu hiyo akisaidiwa na Boniface Mkwasa kama kocha msaidizi .
Kuanza kazi kwa makocha hao kunahalalisha kutimuliwa kwa makocha Wabrazil ambao ni Marcio Maximo na Leonado Neiva.
Aidha Taarifa za ndani ya kikao hicho zimeeleza
kuwa Yanga imeamua kutangaza pia viongozi wapya kwa lengo la kuziba
nafasi zilizokuwa wazi na kuimarisha maeneo yaliyokuwa yanasuasua.
Baadhi ya viongozi waliojiunga na timu hiyo ni Dr
Jonas Tiboroha nafasi ya Katibu Mkuu, Jerry Muro Afisa Habari, Omari
Kaya afisa Masoko, Frank Chacha mwanasheria na Baraka Deusdedit anakuwa
mkuu wa Idara ya Fedha
Jerry Muro Afisa Habari Mpya Wa Timu Ya Yanga
Reviewed by crispaseve
on
09:15
Rating:

Post a Comment