Header AD

Uniongoze’ ya Sekeleti yaingia sokoni

KAMPUNI ya Msama Promotions imeanza rasmi kusambaza Dvd ya Uniongoze ya nyota wa nyimbo za injili nchini Zambia, Ephraim Sekeleti tangu mwezi Novemba mwaka huu. Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama DVD hiyo ina nyimbo nane  ambazo ameziimba katika lugha ya Kiswahili.

Msama alisema hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki wa injili kutoka kwa muimbaji huyo anayetamba na kibao cha ‘Uniongoze’ imeingia sokoni kwa kishindo kutokana na ubora wa albamu hiyo.

Alisema msanii huyo kutoka Zambia alijizolea umaarufu hapa nchini baada ya kushiriki kwenye matamasha ya Pasaka na Krismasi kutokana na uwezo wake wa kumiliki jukwaa pamoja na sauti yake. Msama albamu hiyo ya Uniongoze imetayarishwa na Msama Video Productions na kusambazwa na Msama Promotions ambayo ina ubora wa hali ya juu, hivyo mashabiki na waumini mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujionea kazi zilizofanywa na kampuni hizo.

Aidha Msama alijipambanua kwa kueleza kwamba inapatikaba kwenye maduka ya Msama yaliyopo Kariakoo mtaa wa Masasi na Msimbazi na Posta mtaa wa Mkwepu. Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Uniongoze, Baraka za Mungu, Kidonge cha Yesu, Wewe uko, Ndani ya jina, Kuna wakati Nachoka, Mungu mwenyewe na Ephraim Sekeleti interview.
Uniongoze’ ya Sekeleti yaingia sokoni Uniongoze’ ya Sekeleti yaingia sokoni Reviewed by crispaseve on 04:47 Rating: 5

No comments

Post AD