KITUO CHA RADIO 5 CHAANDAA “KAMPENI YA RADIO 5 VIWANJANI”MSIMU HUU WA SIKUKUU YA XMASS NA MWAKA MPYA
Radio
5 FM 105.7 imeandaa "kampeni ya RADIO 5 viwanjani" katika mkoa wa
Arusha ambapo itawakutanisha watangazaji na madjs na wasikilizaji wao
katika kumbi za starehe kwa takribani wiki tano ikiwa ni sehemu ya
kuwashukuru mashabiki wa Redio hiyo kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima huku
mashabiki wakijipatia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo(katika picha ni
Mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Julius Kamafa aliyejizolea umaarufu
mkubwa jijini Arusha kupitia kipindi chake cha funiko base
kinachosikilizwa zaidi na vijana akishow love na msikilizaji wake katika
kampeni ya "Redio 5 viwanjani"ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda jijini Arusha
Timu kazi ya Redio 5 wakifatilia show
Mtangazaji
maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha love
cuts Semio Sonyo akiwa anauliza maswali kwa vijana wa Arusha waliofika
katika kampeni ya Redio 5 viwanjani ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda jijini
Arusha.
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akifurahia jambo katika kampeni ya Redio 5 viwanjani iliyofanyika jijini Arusha
Mtangazaji
maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha love
cuts Semio Sonyo akimuuliza maswali shabiki wa redio 5 katika kampeni ya
Redio 5 viwanjani yenye nia ya kuwashukuru wasikilizaji wa kituo hicho
kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima.
KITUO CHA RADIO 5 CHAANDAA “KAMPENI YA RADIO 5 VIWANJANI”MSIMU HUU WA SIKUKUU YA XMASS NA MWAKA MPYA
Reviewed by crispaseve
on
06:52
Rating:
Post a Comment