DIAMOND NA DAVIDO HAWANA BIFU ASEMA BABU TALE

Babu Tale amesema wamekuwa na mawasiliano mazuri na
menejimenti ya Davido na hata ujumbe aliouandika Davido kwenye ukurasa
wake wa Twitter uliomsababishia ashambuliwe na watanzania mapema mwaka
jana haukuwa ukimlenga Diamond.
”Mimi na management ya Davido
tunaongea, hata naweza kukuonyesha meseji za mimi na Kamal ambaye ni
meneja wa Davido…na kulingana na….nikunukuu maneno ya Kamal kwangu hata
ile meseji ambayo Davido ambayo alipost ya kwanza They Cheated again….
hakuwa anamface Diamond….according to Kamal…akaniambia mbona watanzania
wameelewa vibaya”, alisema Tale.
Pia amesema hata tweets ambazo ameandika hitmaker huyo wa
Skelewu hivi karibuni hazikuwa zinaamlenga Diamond na kuwataka
watanzania wawe wapole.
”Sitaki kuamini kama Davido na Diamond wana
vita, juzi Davido alikuwa ana-post vitu vyake …sio kwa sababu ya
Diamond…watanzania wote washaanza kusema tena oohh Davido anamtukana
tena Diamond..hakuna sio hivyo”.
Unaweza ukatazama Tweets za Davido alizoandika hivi karibuni
ambazo zimewafanya mashabiki wa Diamond kudhani huenda kukawa na bifu
linaloendelea kati yao.

DIAMOND NA DAVIDO HAWANA BIFU ASEMA BABU TALE
Reviewed by crispaseve
on
21:55
Rating:
Post a Comment