Header AD

LIGHT BAND ILIVYOWABAMBA MASHABIKI WAKE 'VALENTINES'S DAY' NDANI YA THAI VILLAGE


 DSC_0346
Mwanadada mrembo akipozi kwenye eneo maalum kukaribisha mashabiki wa Skylight Band kwa shots za Zappa na Tequila pamoja na ua aina ya Rose maalum kuonyesha upendo kwa wapenzi wao katika usiku maalum wa wapendanao uliofanyika jumamosi iliyopita ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village....Skylight Band itaendelea kusambaza upendo Ijumaa ya leo, baada kurejea nyumbani salama wakitokea nchini Oman....Muda ule ule... uchakavu ule ule... mahali ni pale pale....Karibuni.
DSC_0334
Mkali wa R & B Skylight Band, John Music akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo kwenye usiku maalum wa wapendanao (Valentine's Night Party) iliyofanyika siku ya Jumamosi ikiwa lengo la kusambaza upendo kwa mashabiki wao Valentine's day. Kulia ni Ashura Kitenge na kushoto ni Baby wakipiga back vocal kumsapoti John Music.
DSC_0343
Ashura Kitenge akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band sambamba na kusindikizwa na Baby.
DSC_0393
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akitoa burudani kwa hisia kali ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar kwenye usiku maalum wa wapendanao ulioandaliwa na bendi hiyo. Katikati ni Aneth Kushaba AK47 pamoja na Sam Mapenzi wakimsindikiza Sony Masamba.
DSC_0398
Mashabiki wa Skylight Band wakisakata rhumba siku ya maalum ya usiku wa wapendano nao iliyofanyika ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0401
Rapa mkongwe wa muziki wa Live Joniko Flower akiwachezesha ligwaride waimbaji wenzake kwenye usiku maalum wa wapendanao uliofanyika ndani ya kiota cha Thai Village, mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Sam Mapenzi, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Sony Masamba.
DSC_0409
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiitikia ligwaride la rapa Joniko Flower na style za aina yake.
DSC_0417
DSC_0455
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo kwenye usiku maalum wa siku ya wapendanao sambamba waimbaji wenzake, Kutoka kushoto ni John Music, Baby pamoja na Ashura Kitenge.
LIGHT BAND ILIVYOWABAMBA MASHABIKI WAKE 'VALENTINES'S DAY' NDANI YA THAI VILLAGE LIGHT BAND ILIVYOWABAMBA MASHABIKI WAKE 'VALENTINES'S DAY' NDANI YA THAI VILLAGE Reviewed by crispaseve on 01:49 Rating: 5

No comments

Post AD