MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA DKT. EDWARD HOSEA, JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki
kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo
Feb 27, 2015.

Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika
kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake,
Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji,
Familia ya wafiwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea na nduguze, waliofiwa
na mama yao mzazi wakati Makamu alipofika kushiriki katika shughuli ya kuaga,
Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za
mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi
Mkuu wa Takukuru, Dkt. Ewdard Hose, Mama Esther Gigwa, wakati wa
shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa Mkurugenzi huyo, Masaki
jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA DKT. EDWARD HOSEA, JIJINI DAR.
Reviewed by crispaseve
on
14:26
Rating:

Post a Comment