MSAMA PROMOTIONS LTD YAMWAGA MISAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA, YALAANI MAUAJI YA ALBINO YANAYOENDELEA NCHINI

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex
Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Halima Ramadhan Mlezi wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Tegeta jijini Dar es
salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni moja ya misaada inayotolewa
katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima wakati wa msimu huu
wa maadalizi ya Tamasha la Pasaka linalotimiza miaka 15 tangu
lianzishwe.
Msama
amekabidhi misaada hiyo kwa vituo vitano vya kulelea watoto waishio
katika mazingira magumu,makabidhiano ya misaada hiyo ilifanyika kwenye
ofisi za kampuni hiyo,Kinondoni jijini Dar.
Msama
alisema kuw maandalizi ya tamasha hili yanaendelea vyema mpaka sasa,na
kwamba tamasha hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar April 7
2105,ambapo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa Kimataifa na wa
Nchini,aliongeza kuwa ili kunogesha zaidi tamasha hilo pia kutakuwepo na
michezo mbalimbali itakayochezwa ikiwemo na kukabidhi zawadi na vikombe
kwa washiriki wa tamasha hilo.
katika
hatua nyingine Bwa.Alex Msama amelaani matukio ya mauaji ya Albino hapa
nchini,ameiomba Serikali kutilia mkazo katika janga hilo ambalo
limekuwa likiibua na kuzua gumzo miongoni mwa jamii,hivyo ameiomba
Serikali kuwashughulikia ipasavyo wahusika wote waliofanya na wanaofanya
ukatili huo ambao ni kinyume kabisa na maadili ya nchi yetu,na ikibidi
kukomesha kabisa matukio hayo ambayo yamekuwa yakilitia aibu Taifa letu.

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex
Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael Mlezi wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es
salaam.

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex
Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Rashid Mpinda Katibu wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Mosco
jijini Dar es Sakaam.

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex
Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Soud Said Mwakilishi wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Ijanzo Zanda orphanage Centre cha jijini
Dar es salaam

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex
Msama akiwa amewabeba baadhi ya watoto wa kituo cha Honorata wakati
alipowakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali.
MSAMA PROMOTIONS LTD YAMWAGA MISAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA, YALAANI MAUAJI YA ALBINO YANAYOENDELEA NCHINI
Reviewed by crispaseve
on
08:02
Rating:

Post a Comment