WAZIRI MKUU AAHIDI BWAWA LA KUTUNZIA MAJI NYANZWA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anakubaliana na ombi la
wakazi wa Nyanzwa na Igunda wilayani Kilolo, mkoani Iringa kuhusu ujenzi
wa bwawa la kuhifadhia maji yatakayovunwa msimu wa mvua ili yasaidie
kuongeza eneo la mradi wa umwagiliaji.
Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akiwahutubia
wakazi wa vijiji vya Nyanzwa na Igunda, mara baada ya kukagua mradi wa
umwagiliaji wa Nyanzwa ambao ni maarufu kwa kilimo cha vitunguu.
“Huu mradi ni wa siku nyingi. Nimewauliza wataalamu
niliokwenda nao wakasema ujenzi wa bwawa ndiyo suluhisho pekee la kuokoa
mradi huu na kwamba ni jambo linalowezekana kama fedha zipo.”
Aliutaka uongozi wa mkoa uandae mpango kazi na wauweke
kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha ili mradi huo uweze kuombewa fedha
kwenye bajeti kuu ya Serikali. ia aliwataka wakazi wa eneo hilo
wakitunze chanzo cha maji kwa kuweka mipaka ili watu wasikivamie na
hatimaye kukiharibu.
“Tengeni eneo kwa kuweka mipaka. Mkurugenzi simamia uwekaji
wa mipaka kwenye chanzo hiki ili tukilinde kwani uharibifu wa mazingira
utakiharibu kabisa,” alisisitiza.
Akiwa katika ukaguzi wa eneo la mradi, Waziri Mkuu
alikutana na mkulima mmoja wa vitunguu Bw. Furaha Ngalali (32) ambaye
alimweleza kwamba mwaka jana alifanikiwa kulima ekari tatu za vitunguu
ambazo zilimpatia kiasi cha milioni 6/- huku kila gunia akiwa ameliuza
kwa sh. 70,000/-.
WAZIRI MKUU AAHIDI BWAWA LA KUTUNZIA MAJI NYANZWA
Reviewed by crispaseve
on
08:00
Rating:

Post a Comment