Wadau wa Utamaduni washauriwa kutoiga tamaduni za nchi nyingine

Kaimu
Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Afisa Bw. Habibu Msami akimkaribisha Mgeni rasmi kufunga kikao
kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi.

Mgeni
rasmi wakati wa kufunga kikao kazi cha sekta ya utamaduni akimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.
Raymond Mushi akizungumza na wadau wa utamaduni kuwapongeza kuwa na
ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa
Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa
Bw. Habibu Msami

Afisa
Utamaduni kutoka Kiteto Bibi. Bihawa Masawika akitoa neno la shukrani
wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini
Dar es Salaam.

Afisa
Utamaduni kutoka Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita Bw. Athanas Michael
akiimba shairi la kuhamasisha kudumisha Utamaduni wakati wa kufunga
kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.

Mshairi
kutoka Chama cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) Bw. Issa Amiri
Kilimo akiimba shairi la kuipongeza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo kwa kushirikiana na wadau wa utamaduni kuhamasisha masuala ya
utamaduni wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni
jana Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Utamaduni washauriwa kutoiga tamaduni za nchi nyingine
Reviewed by crispaseve
on
12:14
Rating:
Post a Comment